Joy FM

Wananchi wapongeza zahanati kukamilika Kakonko

3 March 2026, 10:44

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Bi Asha Kwariko, Picha na Lucas Hoha

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Kigoma kwa kushirikiana na World Vision imefanikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kabale Wilayani Kakonko na kusaidia upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi

Na Lucas Hoha

Wananchi wa Kijiji cha Kabale Kata ya Gwarama Halmashauri ya Wilaya ya Kankonko Mkoani Kigoma wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya baada ya TAKUKURU Mkoa wa Kigoma kufanikisha ujenzi wa Zahanati yenye thamani ya shilingi milioni 246.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Bi Asha Kwariko wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utendaji kazi wa Takukuru katika kipindi cha Oktoba  hadi Disemba 2025.

Sauti ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Bi Asha Kwariko
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Bi Asha Kwariko, Picha na Lucas Hoha

Wakati huohuo Kwariko amesema Takukuru Mkoa wa Kigoma imefuatilia  miradi 27 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 7 na kwamba wakati wa ufuatiliaji walibaini mapungufu mbalimbali ikiwemo baadhi ya majengo ya vyumba vya madarasa kujengwa tofauti na michoro ya wizara.

Sauti ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Bi Asha Kwariko

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamesema Takukuru kufuatilia miradi ya maendeleo inasaidia kupunguza vitendo vya rushwa kwenye miradi nakusaidia miradi kujengwa kwenye ubora kulingana na fedha iliyotolewa.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Bi Asha Kwariko, Picha na Lucas Hoha

Wananchi wanatakiwa kubadili mtazamo wa kuliona jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa kuwa ni la Takukuru peke yake bali wawe na wajibu wa uzalendo kwa Taifa lao nakupambana dhidi ya vitendo vya rushwa.