Joy FM
Joy FM
3 March 2025, 15:15

Askofu Mkuu wa Kanisa la FPCT Tanzania amesema viongozi wa dini hawana budi kusimama imara na kuwa waadilifu katika kuwatumikia waumini wao.
Na Hagai Ruyagila
Viongozi wa dini katika Kanisa la FPCT Jimbo la Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuwa waadilifu kwa kumtegemea Mungu ili kuwa kioo katika jamii inayowazunguka.
Ni katika ibada maalumu ya Kanisa la FPCT Kasulu Mjini ibada ambayo imeongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la FPCT Tanzania Askofu Steven Mulenga wakati wa kusimika viongozi mbalimbali wa Jimbo la Kasulu.

Askofu Mulenga amesema kiongozi wa dini unatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na katika kazi unayoifanya sambamba na kuepuka mafundisho ya mitandaoni badala yake kumshirikisha Mungu katika maandalizi ya Neno la Mungu kwa ajili ya kuiweka jamii pamoja.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Kasulu Sabato Kigongo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuilinda amani tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa serikali ifikapo mwezi oktoba mwaka huu.

Naye Askofu wa jimbo la Kasulu Shedrack Bunono amesema kama viongozi waliochaguliwa wanahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa waumini ili kuongeza maendeleo zaidi waweze kuendelea kuihubiri injili ambayo itawasaidia watu kumjua Mungu sanjari na kubadili maisha yao yaweze kumpendeza Mungu.