Joy FM

Wanawake wahimizwa kuwania nafasi za uongozi

9 September 2024, 15:21

Baadhi ya viongozi wa shirika la LEGAL AID SHARE AND CARE FOR ALL, wakiwa na wanawake baada ya semina ya uongozi, Picha na Lucas Hoha

Wanawake Mkoani Kigoma wameshauriwa kujitokeza kushiriki na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jamii hasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Na Luca Hoha – Kigoma Dc

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu na uchaguzi mkuu hapo mwakani, Wanawake Mkoani Kigoma wametakiwa kujitokeza kushiriki kikamilifu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Hayo yameelezwa katika hafla yauzinduzi wa mradi wa kuhamasisha  usawa wa kijinsia kushiriki kwenye siasa na uongozi  unaoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la LEGAL AID SHARE AND CARE FOR ALL yani  LASCA linalojihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kutoa msaada wa kisheria na kupinga ukatili wa kijinsia  lililopo Wilaya ya Kigoma

Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya kigoma ambaye pia ni kaimu mratibu wa mashirika yasiyo ya kiserika  George Vansauli ametumia nafasi hiyo kuwataka wanawake kujiamini kuwa wanao uwezo wa kuongoza, huku akiitaka jamii kuacha mfumo dume wa kuwakandamiza wanawake katika masuala ya uongozi na  siasa.

Story ya Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya kigoma ambaye pia ni kaimu mratibu wa mashirika yasiyo ya kiserika  George Vans.

Kwa upande wake, mratibu wa mradi huo kutoka shirika la LASCA lililopo Wilaya ya Kigoma  John Kamaliza Ntabagala amesema wameamua kutekeleza mradi huo kwa sababu asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa hawajitokezi kwenye masuala ya siasa kutokana na sababu mbalimbali za kijamii ikiwemi mila na desturi zinazowakandamiza wanawake.

Sauti ya mratibu wa mradi huo kutoka shirika la LASCA lililopo Wilaya ya Kigoma  John Kamaliza Ntabagala.

Nao baadhi ya wanawake ambao wameshiriki uzinduzi wa mradi huo wamesema wamehamasika kushiriki kwenye masuala ya uongozi na siasa na kutaja baadhi ya majukumu yanayowafanya wasishiriki ikiwemo majukumu ya familia.

Sauti ya wanawake ambao wameshiriki uzinduzi wa mradi huo