Joy FM

Baraza la madiwani kibondo lapitisha rasmu ya bajeti ya bilioni 37.9

2 February 2024, 09:28

Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo Habili Maseke na baadhi ya wajumbe wakati wa baraza la bajeti, Picha na James Jovin

Halmashauri ya Wiliya Kibondo Mkoani Kigoma yapitisha rasmu ya bajeti ya mwaka 2024/2025.

Na James Jovin.

Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma limepitisha rasimu ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 37.9 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 zitakazotumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akitoa taarifa hiyo katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kibondo afisa mipango Bi. Fatna Maya amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia miongozo ya kitaifa na halmashauri.

Aidha amesema  kuwa bajeti hiyo imepitishwa baada ya kupokea ushauri na maoni ya wajumbe  mbali mbali kutoka katika kamati ya ushauri ya wilaya, madiwani na baraza la wafanyakazi.

Sauti ya mwandishi wetu James Jovin akiripoti juu ya bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Kibondo

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Habili Maseke ameitaka idara ya mipango kuhakikisha miradi yote ya halmashauri kuwekwa kwenye vyanzo vya mapato ili kuboresha ufaninisi na utendaji kazi na kuongeza vyanzo vya mapato.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amepongeza baraza la madiwani na watumishi wa halmashauri kwa kazi nzuri wanayofanya lakini pia akiwataka kuendelea kuibua vyanzo vingine vya mapato ili kukuza uchumi wa halimashauri na taifa kwa ujumla.