Joy FM

Mkuu wa wilaya Buhigwe awataka wanaume kuacha kunyonya maziwa ya mama

14 September 2023, 18:27

Baadi ya wananchi wakiwa katika mkutano unaohusu elimu ya masuala ya unyonyeshaji, Picha na Kadislaus Ezekiel.

Baadhi ya Wanaume Katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, wametuhumiwa Kunyonya Maziwa ya Wenza wao wa Ndoa baada ya kujifungua, hali ambayo imechangia watoto kukosa maziwa ya kutosha.

Na, Tryphone Odace

Mkuu Wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina, akizungumza Wakati wa mkutano wa kuhamasisha masuala ya unyonyeshaji, amewataka kuacha mara moja na kusisitiza kina mama kunyonyesha watoto kwa kipindi cha miezi sita bila kuwapa chakula, na kuwataka wanaume kujali malezi ya familia.

Baadhi ya wanawake Wilayani Buhigwe, wanadai kazi za shambani na maisha duni kwa baadhi yafamilia, imepeleeka washindwe kunyonyesha watoto wao kwa mpangilio na hivyo baadhi ya watoto kupata na magonjwa mbalimbali.

Mganga Mkuu Wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Daktarai Innocent Mhagama, Amesema wanaume wanawatwika majukum mengi wanza wao wa ndoa, na kupelekea wengi wao kushidwa kunyonyesha watoto kwa utalatibu.