Joy FM

Kituo cha afya kipya chazinduliwa halmashauri ya wilaya Kibondo

5 January 2024, 17:02

Halmashauri ya wilaya ya Kibondo imezindua kituo kipya cha afya kilichopo katika kata ya Kibondo mjini kilichogharimu shilingi milioni 500 mpaka kukamilika kwake ikiwa ni mkakati wa kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya na  kuboresha huduma za afya.

Na, James Jovin

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha afya Dr. Elizabeth Ntabaye  kwa niaba ya mganga mkuu wa wilaya ya Kibondo amesema kuwa kwa sasa kituo hicho cha afya kitaanza kutoa huduma za nje yaani wagonjwa wanaotibiwa na kuondoka huku huduma zaidi zikiendelea kuboreshwa. 

Dr. Elizabeth amesema kuwa tayari huduma muhimu hasa kwa watoto, wajawazito na wazee zimeanza kutolewa katika kituo hicho cha afya na kwamba wahudumu waliopangwa wanaendelea na mafunzo ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Dr Elizabeth Ntabaye

Katibu wa jimbo la Muhambwe Bi. Doris Nsekela akimwakilisha mbunge wa jimbo hilo katika uzinduzi huo amewataka watumishi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa na kufuata miongozo ya wizara ya afya.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kibondo mjini bw. Alex Baragomwa amesema kuwa kukamilika kwa kituo hicho cha afya kibondo mjini ni tumaini kubwa kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo jirani waliokuwa wakitumia muda mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali ya wilaya ya kibondo kutokana na msongamano mkubwa wa wa wagonjwa

Nao baadhi ya wanananchi waliohudhulia uzinduzi huo wameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika maeneo mbali mbali kote nchini