Joy FM

Watu sita mbaroni matukio ya uvunjaji, wizi Kigoma

13 September 2023, 14:04

Kamanda wa Jshi la Polisi Mkoani Kigoam ACP, Filmon Makungu, Picha na Google

Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma wakituhumiwa kufanya uhalifu na wizi katika maeneo mbalimbali mkoani wa Kigoma.

Na, Kadislaus Ezekiel.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, limethibitisha kuwakama watu sita wakituhumiwa kujihusisha na matukio ya uvunjaji na wizi katika maeneo ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Filemon Makungu amesema, watu hao wamekamatwa kufuatia doria ya kuzuia uhalifu na wahalifu ambapo watu hao wamekutwa na vitu mbalimbali bila kuwa na nyaraka za umiliki.

Akizungumzia matukio yanayofanywa na madereva bodaboda, Kamanda Makungu amesema wamemkamata mtuhumiwa mmoja, kwa kujihusisha na uporaji wa mikoba na simu, wakati mtu mwingine akiendelea kutafuta.

Akizungumzia udhibiti wa dawa za kulevya Kamanda Makungu amesema, Jeshi la Polisi limewakamata watu watano kwa kukutwa na pombe ya moshi wakati wengine saba wakikamatwa kwa kukutwa na kete.