Joy FM

Madereva wafikishwa mahakamani na kufutiwa leseni Kigoma

14 December 2023, 16:54

Madereva wa vyombo vya moto Mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani hasa kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka ili kuzuia ajali ambazo zinaweza kujitokeza.

Na Josephine Kiravu

Akizungumza na wanahabari hivi Karibuni Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Philemon Makungu amesema jumla ya makosa 3,810 ya usalama barabarani yamekamatwa na kutozwa faini na  madereva 4 wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya usalama barabarani.

ACP Philimon Makungu

Kwa upande wao, Baadhi ya madereva katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamekiri kuwepo kwa uzembe kwa baadhi yao wanapokuwa barabarani huku wakisema mwaka huu wamejidhatiti kuumaliza salama bila ya kuwepo kwa ajali ya barabarani.

Madereva

Hata hivyo Kamanda Makungu amesema wanaendelea kuchukua  hatua mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa magari ya abiria, utoaji elimu kwa watumiaji wa barabara wakiwemo madereva, abiria na waenda kwa miguu.