Joy FM

Watu 29 mbaroni kwa tuhuma za ramli chonganishi Mkoani Kigoma

18 July 2023, 16:16

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma ACP Philemon Makungu akionyesha baadhi ya vifaa vya ramli, Picha na Josephine Kiravu.

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limesema litaendelea kutoa elimu kwa jamii kuachana na vitendo vya ramli chonganishi ambavyo husababisha uvunjfu wa amani.

Na, Josephine Kiravu

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhumiwa  29 wakiwa na vifaa vya kufanyia ramli chonganishi katika maeneo ya Kalalangabo kata ya Kibirizi pamoja na maeneo jirani ya mwambao mwa ziwa Tanganyika.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Philemon Makungu amethibitisha kukamatwa kwa wapiga ramli hao ambao wanatajwa kuwa chanzo cha migogoro na uhalifu ndani ya jamii ikiwemo mauaji na ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya vifaa vya ramli chonganishi vinavyotumiwa na waganga wa jadi, Picha Josephine Kiravu
Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma

Kamanda Makungu amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wasiendelee kuwapokea wapiga ramli chonganishi kwani watu hao wapo kwa ajili ya kujipatia fedha na si vinginevyo.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma

Na hizi zinatajwa kuwa huenda ni chanzo cha wananchi kuhitaji huduma ya ramli chonganishi kutoka kwa waganga hao kama anavyoeleza mkazi huyu wa Katombo Kata ya Mgaraganza.

Baadhi ya vifaa vya ramli chonganishi Picha na Josephine Kiravu

Hata hivyo Jeshi la Polisi limeendelea kukemea vitendo hivyo vya ramli chonganishi Mkoani Kigoma na kwamba atakaebainika kujihusisha ama kuwakaribisha waganga hao hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

Kamanda wa Polisi ACP Philemon Makungu akionyesha vifa vinavyotumiwa na waganga wa jadi kupiga ramli chonganishi, Picha na Josephine Kiravu