Joy FM

Mawasiliano wilayani Buhigwe ni changamoto kubwa

12 January 2024, 16:32

Halmashauri  ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, na Baadhi ya Maeneo ya Wilaya Zinazopakana na Nchi Jirani za Burundi na Congo, zinakabiliwa na Changamoto ya mawasiliano kwa kuwa na Mwingiliano na Nchi Hizo hatua inayokwamisha  ufanisi  katika utendaji kazi kwa kukosa uhakika wa mawasiliano.

Na, kadislaus Ezekiel

Wananchi Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina wameeleza kero hiyo, mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea wakati akikagua kituo cha mkongo wa Taifa kinachojengwa Wilayani Buhigwe ambacho kipo mbioni kukamilika.

Kwa upande wake, Mhandisi wa miundombinu ya Tehama Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Brayan Kaduma akitoa taarifa ya ujenzi wa Kituo cha mkongo wa Taifa Buhigwe, amesema kukamilika kituo hicho kitaondoa kero hiyo.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea, amewafuta machozi wananchi na Viongozi kwa kuagiza Kituo hicho kikamilike mara moja na kuanza kuhudumia wananchi ili kuwaondolea kero ya mawasiliano.

.