Joy FM

Zaidi ya wasichana elfu 23 kupewa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi

22 April 2024, 15:42

Mhudumu wa afya Kasulu akimchoma sindano ya chanjo ya saratani ya malngo wa kizazi mwanafunzi, Picha na Emmanuel Kamangu

Zoezi la utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi unatajwa kuwa mwarobaini wa kuwakinga watoto wa kike dhidi ya saratani ya kizazi kutokana na kwamba ugonjwa huambukiza kwa njia ya kujamiana.

Na Emmanuel Kamangu – Kasulu

Zaidi ya wasichana elfu 23 wa  kuanzia umri wa miaka 9-14 katika halmashauri ya mji wa kasulu wanatarajia kupewa chanjo ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na zoezi litadumu kwa takribani siku tano.

Akizungumza na baadhi ya wananfunzi wa shule za msingi ambao wamefika katika kituo cha afya kiganamo kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kasulu Bw. Nurfus Azizi ambaye amekuwa mbeni rasmiĀ  katika hafara ya uzinduzi wa zoezi la chanjo ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ameiomba jamii nzima kuwapa ushirikiano wataalamu wa afya wakati wanapotekeleza zoezi hilo.

Baadhi ya viongozi akiwemo mratibu wa chanjo kasulu wakiwa kwenye picha na wanafunzi ambao wamejitokeza kupatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi, Picha na Emmanuel Kamangu

Kwa upande wake msimamizi wa zoezi la utoaji chanjo ambaye pia ni muuguzi mkuu mkoani kigoma Bi Esta Kondo amesema ngono isiyo salama imekuwa ni moja ya sababu kubwa ya kusababisha kuongezeka kwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi hivyo ni vema wasichana kupewa kinga mapema.

Aidha Mganga mkuu halmashauri ya mji wa kasulu dk peter janga amesema ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi umekuwa ni moja ya magonjwa hatari sana kwa wanake hasa wanwake wa umri  40 hivyo serikali imezamilia kukabiliana na ugonjwa huo .

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi ambao wamepata chanjo wameishukuru serikali kwa kuona kuna kila sababu za kutoa chanjo ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.

Baadhi ya wanafunzi wilayani kasulu wakipata elimu ya umuhimu wa chanjo ya saratani ya kizazi, Picha na Emmanuel Kamangu

Hata hivyo Mratibu wa chanjo halmashauri ya mji wa kasulu Bi, Itumbe Munis pamoja na mratibu wa elimu ya afya kwa uma Bw, maregela lukiko wamesema chanjo hiyo ni salama hivyo hawatarajii kuona baadhi ya wazi na walezi wanapata kigugumizi kuwaruhusu watoto wao kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.