Joy FM

Afariki baada ya kufukiwa na kifusi cha mawe Kigoma

6 October 2023, 16:21

Mashuhuda waliofika kwa ajili ya kutoa msaada kwa kijana alifunikwa na kifusi cha udongo wakati akichimba mawe, Picha na Eliud Theogenes

Jamii imeomba Serikali kuchukua hatua za kudhibiti shughuli za uchimbaji wa madini ya mawe katika eneo la masanga manispaa ya kigoma Ujiji kutokana na kuhatarisha maisha ya watu.

Na Eliud Theogenes

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Shabani amefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati akichimba mawe katika mgodi wa mawe uliopo katika Mtaa wa Masanga Kata ya Gungu Manispaaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza na Kituo hiki Ndugu wa marehemu Bw. Adam Mikidadi, anaeleza namna  mauti ilivyomfika Shabani huku baadhi ya wananchi wakiomba hatua zichukuliwa ili usalama uwepo.

Baadhi ya mashuhuda wakiwa katika kifusi cha mawe kilichomfunika kijana ambaye alikuwa anachimba kokoto, Picha na Eliud Theogenes

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mgodi huo anaelezea kiundani namna tukio lilivyotokea.

Mwenyekiti wa mtaa wa Masanga kata ya Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji anathibitisha namna Ajali ilivyotokea na anaiomba serikali kuingilia kati suala hilo na kuwa hilo ni tukio la pili ndani ya mwezi mmoja.

Hata hivyo Jeshi la polisi limefanikiwa eneo la kuondoka mwili wa marehemu kwa ajili ya  kuendelea na taratibu nyingine za kiuchunguzi.