Joy FM

Zaidi ya watoto 884,500 kupatiwa chanjo ya polio Kigoma

8 September 2023, 13:34

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Albert Msovela akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa wahudumu ngazi ya jamii, Picha na Josephine Kiravu.

Na, Josephine Kiravu

Zaidi ya watoto 884,500 walio chini ya miaka 8  wanatarijiwa kufikiwa na kupatiwa chanjo ya Polio ambayo itaanza kutolewa nyumba kwa nyumba kuanzia septemba 21hadi 24 Mkoani Kigoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa kamati ya msingi ya afya ngazi ya jamii (PHC) Mkoa wa Kigoma Katibu Tawala MKoani hapa Albert Msovela amesema ili kufanikisha kampeni hii jamii inapaswa kushirikiana vyema na watoa huduma za afya ili watoto wote walengwa wafikiwe kwa urahisi.

Sauti ya Katibu tawala Kigoma
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao cha kujadili kampeni ya polio Mkoani Kigoma, Picha na Josephine Kiravu.

Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Dr. Jesca Leba ameeleza mikakati ya Mkoa katika kufanikisha kampeni hii ambapo amewataka wazazi kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya Polio.

Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa chanjo Mkoa wa Kigoma Deltus Sevelin amesema ugonjwa wa polio una madhara mengi kwa watoto ikiwemo kupooza na kusababisha ulemavu na hapa anatoa ufafanuzi kuhusu chanjo zitakazotolewa kwa watoto chini ya miaka 8.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala mKoani Kigoma Albert Msovela amewataka wazazi kuzingatia usafi kwa watoto wao ili kudhibiti ugonjwa wa kuharisha kwa watoto ambapo kuanzia julai 14 mpaka kufikia September 07 mwaka huu watoto zaidi ya 1552 waliugua ugonjwa huo na watano kati yao walipoteza maisha na waliougua ni watoto chini ya miaka 5.