Joy FM

Manispaa ya Kigoma Ujiji yapunguza kiwango cha utapiamlo

14 September 2023, 16:24

Akina mama wakifundishwa na namna ya kuanda uji wa lishe kwa watoto, Picha na Josephine Kiravu

Wazazi na walezi Manispa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia lishe kwa watoto wao kwa kuanda na kuwalisha vyakula vye lishe ya kutosha ili kuwakinga na utaopiamlo.

Na, Josephine Kiravu

Tangu kuanzishwa kwa siku ya afya ya lishe kila baada ya robo mwaka kwa Mitaa na vijiji, Manispaa ya Kigoma Ujiji imefanikiwa kupunguza kiwango cha Utapiamlo kutoka aslimia 43 mwaka 2019 hadi asilimia 21 kwa takwimu za mwaka 2022.

Wananchi wakipata elimu ya lishe Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Josephine Kiravu

Hayo yameelezwa na Afisa Lishe Manispaa ya Kigoma ujiji, Omary Kibwana ambapo amesema licha ya kufanikiwa kupunguza utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano bado baadhi ya watoto wanapoteza maisha, na kuwataka wazazi kuzingatia lishe bora ili kunusuru maisha ya watoto wao.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi waliofika kwenye ofisi za Serikali ya mtaa wa buteko kata ya Bangwe wameeleza faida za siku ya afya ya lishe ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuandaa lishe bora kwa watoto wao.

Sufuria la uji wa lishe ambao unatumika kuwafundishia akina mama namna ya kuanda uji wa lishe.

Kumbuka tu ewe mzazi/mlezi endapo utazingatia elimu ya lishe na kuitekeleza kwa voitendo, tatizo la udumavu, na utapiamlo pamoja na maradhi mengine yatokanayo na lishe duni yatapungua na kuwa na jamii yenye afya bora.