Joy FM

Madiwani watakiwa kusikiliza kero za wananchi Kasulu

29 March 2024, 10:53

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Mberwa Chidebwe amewaagiza madiwani wote wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu kusikiliza kero za wananchi ili ziweze kutatuliwa na serikali kuliko kusubiri viongozi wa kitaifa.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo, viongozi wa dini, kamati ya ulinzi na usalama wa wilayani ya Kasulu, pamoja na viongozi wa vyama vya siasa katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu.

Amesema bila kujali itikadi ya vyama vyao ni vizuri kuwa na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi ili ziweze kutatuliwa na viongozi waliopo kuliko kusubiri viongozi wa kitaifa waje kutatua kero hizo

Katika hatu nyingine Chidebwe amewaomba madiwani kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi mpya wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu katika juhudi za kuiletea serikali maendeleo.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo akiwemo Mathias Sunzu kutoka Buhoro, Fabiano Dangi Dolage kutoka Rusesa, Julius Yosam kutoka Asante Nyerere na Relata Rihange wa viti maalum wamesema ni wajibu wao kutoa ushirikiano na kusikiliza kero za wananchi ili halmashaauri hiyo isonge mbele katika suala zima la maendeleo.