Joy FM

Watoto zaidi ya 600 waripotiwa kufariki wakati wa kuzaliwa Kigoma

5 January 2024, 16:43

Zaidi ya watoto wachanga 600 wamefariki wakati wa kuzaliwa mkoani Kigoma huku akina mama 76 wakipoteza maisha wakati wa kujifungua  katika  kipindi  cha Januari hadi  Desemba 2023.

Na, Josephine Kiravu.

Hakuna mama anaebeba ujauzito kwa kipindi cha miezi 9 halafu matarajio yake yakawa sio kumpokea mtoto, mama yeyote anatamani mwisho wa ujauzito wake apakate kichanga wake na afurahie.

Lakini hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya akina mama kwani wamekuwa wakipoteza watoto na wengine kupoteza uhai wao wakati wa kujifungua kama anavyotueleza Kaimu mganga mkuu mkoa wa Kigoma Abeid Michael.

Sauti :Abeid Michael

Hata hivyo katika kukabiliana na tatizo hili Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Thamini Uhai wametoa mafunzo kwa wanahabari 10 kutoka Mkoa wa Kigoma na Katavi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza vifo vya watoto wachanga na akina mama wakati wa kujifungua.

Sauti :Abeid Michael

Lakini je baadhi ya wanahabari ambao pia ni wazazi wanazungumziaje tatizo hili la vifo vya watoto wachanga na akina mama wakati wa kujifungua?

wanahabari

Hebu sikiliza simulizi hii kutoka kwa Irene Temu mama wa watoto 3 huenda wewe mama uliepoteza mtoto ukapata faraja na kama tayari ni mjazito utapata faraja kwanza alipokelewaje alipokwenda kujifungua.

Irene Temu

Mama mjamzito jitahidi kuwahi hospitali mapema uonapo dalili za hatari ili uweze kupewa msaada, Pia muda wako wa kujifungua ukifika wahi mapema hospitali ili kuepuka kujifungulia nyumbani au barabarani pindi uelekeapo hospitali, kwasababu kuna matatizo mengi yatoka nayo na kujifungua ivyo ukijifungulia nyumbani au barabarani kuna uwezekanao  mkubwa  wa  kupoteza  maisha yako, lakini ukiwahi hospitali utasaidiwa hata kama matatizo yatakapojitokeza utakuwa salama.”Ewe mama mjamzito   unayetarajia  kujifungua  chukua hatua kujifungua salama inawezekana.”