Joy FM

Sababu ya kutoa chanjo ya polio watoto chini ya miaka 8 yabainishwa

25 October 2023, 16:07

Zaidi ya watoto Laki tatu na elfu hamsini wenye umri chini ya miaka 8 Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya polio awamu ya pili ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.

baadhi ya wadau wakiwa katika kikao cha maandalizi ya kampeni ya kuzuia ugonjwa wa polio awamu ya pili, Picha na Hagai Ruyagila.

Na, Hagai Ruyagila

Hayo yamebainishwa na katibu tawala wilaya ya kasulu Theresia Mtewele wakati akimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo Kanal Isaac Mwakisu kwenye ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya kampeni ya kuzuia ugonjwa wa polio awamu ya pili itakayofanyika novemva 02 hadi 05 mwaka huu.

Amebainisha idadi ya watoto wanaokwenda kupatiwa chanjo hiyo ni wenye umri chini ya miaka 8 na zoezi hilo litafanyika kwa kila halmashauri iliyopo mkoani Kigoma huku akibainisha moja ya sababu ya kutoa chanjo hiyo ni kutokana na baadhi ya nchi jirani kukumbwa na janga hilo la ugonjwa wa polio.

Katibu Tawala Theresia Mtewele

Kwa upande wake, Mratibu wa chanjo halmashauri ya Kasulu Mji Itumbe Munisi amesema tayari wamepokea chanjo ya matone ya polio licha ya kuvuka lengo kwa kupata asilimia 129 katika chanjo ya awamu ya kwanza

Mratibu wa chanjo kasulu TC Itumbe Munisi

Naye mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya kasulu Eliah Thomas amesema licha ya kuvuka lengo la utoaji wa chanjo ya polio awamu ya kwanza kwa asilimia 116 amebainisha mikakati ya kuwafikia wale wachache ambao walikosa chanjo awamu ya kwanza

Mratibu wa chanjo kasulu DC Eliah Thomas

Hata hivyo zoezi la utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 awamu ya pili inatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Songwe, Mbeya, Kigoma na Kagera.