Joy FM

DC Kasulu: Mnafanyia kazi mahali pachafu

25 April 2024, 16:05

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu akizungumza na wahudumu wa afya wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Natamani kuona juhudi za serikali inazofanya kuboresha majengo ya vituo vya afya zinatumika pia kwenye kusimamia usafi ili wananchi wapate huduma mahali pasafi sio mgonjwa anakutana na uchafu hawezi hata kupona.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac mwakisu amewaagiza makatibu wa afya katika vituo vya afya, Zahanati na Hospitali wilayani  humo kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya Vinakuwa safi muda wote  na kutenga siku maalumu za kufanya usafi.

Amesema hayo wakati akizungumza katika kikao kazi na wahudumu wa afya wa halmashauri za mji kasulu na halmashauri ya wilaya ya kasulu chenye lengo la kubaini changamoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ili ziweze kutaftiwa ufumbuzi.

Kanali Mwakisu amesema suala usafi ni jukumu la kila mmoja hivyo makatibu wa afya wametakiwa kusimamia na kuhakikisha mazingira ya hospitali,zahanati na vituo vya afya yanakuwa safi muda wote na kuepuka kutegemea makampuni ya usafi pekee.

Sauti ya mkuu wa wilaya Kasulu kanali Isac Mwakisu

Aidha kanali mwakisu ameongeza kuwa kuelekea katika maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanzania waganga wakuu wa halmashauri wanatakiwa kuhakikisha vituo vya kutoa huduma za afya vinakuwa safi ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Sauti ya Mkuu wa wilaa kasulu Mkoani Kigoma

Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya mji kasulu dkt.Peter janga pamoja na kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya kasulu dkt Mageni pondamali wamesema watasimamia zoezi hilo na kwamba wametenga kila siku ya jumamosi kuwa ni siku ya watoa huduma za afya kufanya usafi katika vituo vyao.