Joy FM

Hatua kali kuchukuliwa watoto kutoripoti shuleni

17 January 2024, 09:54

Mkuu  wa Wilaya  ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amewataka Wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti shule wahakikishe wanakwenda shule kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Na Hagai Luyagila

Kanali mwakisu amesema mahudhurio ya wanafunzi shuleni bado hayaridhishi hivyo ni vyema watoto wakapelekwa shuleni ili wapate elimu itakayowasaidia katika maisha yao.

Aidha Kanal Mwakisu amesema endapo mtoto hana unifomu ataruhusiwa kuvaa nguo hata za sikukuu zilizopita huku mzazi akiendelea kujipanga kumnunulia.

Kwa upande wake Mhashamu Askofu wa dayosisi ya western Tanganyika Emmanuel Bwatta amesema wataungana na serikali kuhakikisha wana wahamasisha wazazi ambao hawajawapeleka watoto kuripoti shule.

Nao baadhi ya wazazi na walezi wa wilaya ya Kasulu akiwemo Joan Lumenyela, Josephine Shemu na Silivanus Buhengeli wamesema serikali iwafatilie wazazi wote ambao watoto wao hawajaripoti shule ili wajuwe nini tatizo