Joy FM

Wananchi walia na ubovu wa miundombinu ya barabara kigoma

29 February 2024, 13:06

Ujenzi wa daraja katika barabara ya Kwitanga inayotokea mahembe hadi Buhigwe ukiendelea, Picha na Orida Sayon

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara hali ambayo imewalazimu wananchi kupaza sauti kwa serikali kuwasaidia kukarabati barabara kwenye maeneo yao.

Na, Orida Sayon

Wananchi wa Kata ya Kalinzi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara katika kata hiyo hali inayosababisha washinde kufanya shughuli za uzalishaji kupitia usafirishaji.

Wameeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya kalinzi ikiwa ni mwendelezo wa mikutano inayoendeshwa na Mkuu wa Wilaya Kigoma kupitia kliniki ya kusikiliza kero za wananchi ambapo wameeleza kuwa ubovu barabara kutoka kalinzi hadi matyazo na eneo la kwitanga imekuwa ikikwamisha shughuli za maendeleo katika vijiji hivyo.

Sauti ya wananchi wa kata ya Kalinzi

Naye Meneja wa wakala wa barabara za mijijina vijijini (TARURA) Wilaya ya Kigoma Mhandisi Augustino Magere amesema kuwa uwepo wa mvua nyingi umepelekea ucheleweshwaji wa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizo na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu hadi mwezi may 2024.

Sauti ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Kigoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh.Salum Kali amemtaka meneja wa TARURA Mhandisi Augustino Magelle kuhakikisha anasimamia uboreshaji wa barabara hizo na ujenzi wa daraja katika kipande cha barabara kutoka kalinzi hadi kwitanga kukamilika kwa wakati .

Mkuu wa Wilaya Kigoma Salum Kalli akikagua ujenzi wa daraja katika barabara ya Kwitanga, Picha na Orida Sayon
Sauti ya Mkuu wa Wilaya Kigoma Mh. Salum Kalli

Katika hatua nyingine, mmoja wa wafanya biashara na mwananchi wa kijiji cha kalinzi Aneth Robison ametoa kero kwa vyombo vya moto kutofuata alama za usalama barabarani eneo la soko la kalinzi na kuiomba serikali  kuboresha usalama kuepuka ajali zinazotokea hasa siku za minada katika soko hilo .