Joy FM

Viongozi wa dini wajadili mustakabali wa malezi na matunzo ya mtoto nchini

9 August 2023, 12:43

Naibu Katibu mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalum Amon Mpanju, Picha na Josephine Kiravu.

Vitendo vya ukatili katika jamii vimetajwa kuchochewa na uwepo wa mmomonyoko wa maadili hali ambayo inatajwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wazazi ambao hawatimizi wajibu wao ipasavyo kwa watoto.

Na Josephine Kiravu

Viongozi mbalimbali wa dini kutoka mikoa ya Kanda ya magharibi nchini Tanzania wamekutana Mkoani Kigoma ikiwa ni mkakati wa kuunda mustakabali wa kuhakikisha wazazi na walezi wanatimiza wajibu wao katika Malezi na matunzo ya mtoto lengo likiwa ni kuondoa mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Akifungua warsha hiyo ambayo inatarajia kudumu kwa takribani siku nne Naibu Katibu mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalum Amon Anastaz Mpanju amewataka viongozi wadini kuwahimiza wazazi na walezi kutimiza wajibu kwa watoto wao kwa kuwapatia mahitaji Yao ya msingi ili kujenga kizazi kilicho Bora na kuondoa ukatili wa kijinsia kwa watoto kwenye jamii.

Naibu Katibu mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalum Amon Mpanju, Picha na Josephine Kiravu.
Sauti ya Naibu katibu mkuu Wizara ya maendeleo ya jamii na makundi maalum, Amon Mpanju

Ameongeza kuwa viongozi wa dini wanayo nafasi ya kutengeneza kizazi hiki kwa kutumia maandiko ya dini na kuzuia visababishi vya mmomonyoko wa maadili ikiwemo utelekezaji wa familia kwa kisingizio cha umasikini pamoja na kuzuia ukatili unaofanywa na ndugu wa karibu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya mtoto Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na Makundi maalum Sebastian Kitiku amesema ipo haja ya jamii kujengewa uwezo wa namna ya kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji na ukatili ambao umekuwa ukishuhudiwa kwenye jamii.

Mkurugenzi Idara ya mtoto Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na Makundi maalum Sebastian Kitiku.
Sauti ya Mkurugenzi Idara ya mtoto Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na Makundi maalum Sebastian Kitiku.

Nao baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria warsha hiyo akiwemo Askofu Jimbo Katoliki Kigoma Joseph Mlola pamoja na Shekhe Mkuu Mkoa wa Dodoma Shekh Shabaan wamesema ili kurudisha maadili kwenye jamii ni lazima kusimamia vyema mafundisho ya ndoa kwani wazazi wengi wamekuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto.

Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria warsha hiyo akiwemo Askofu Jimbo Katoliki Kigoma Joseph Mlola pamoja na Shekhe Mkuu Mkoa wa Dodoma Shekh Shabaan, Josephine Kiravu
Sauuti ya viongozi wa Dini Kanda ya magharibi

Kwa upande wao waratibu wa warsha hiyo ambayo ni UNICEF wamesema jukumu lao ni kuhakikisha Taifa linakuwa imara hivyo kupitia viongozi Hawa wa dini wanaamini jamii itapata elimu na wazazi/walezi watatimiza wajibu wao kwa katika Malezi na matunzo ya mtoto.

Sauti ya Mwakilishi wa UNICEF

Warsha hii ambayo imeanza hii Leo imewamutanisha viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali kutoka mikoa ya Singida, Manyara, Tabora, Katavi,Dodoma na Kigoma.