Joy FM

kamati ya siasa ccm kigoma yaridhishwa na maboresho ya ofisi za KUWASA

11 January 2024, 13:15

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma imetembelea ofisi za Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Kigoma (KUWASA) kwa lengo la kukagua ukarabati wa ofisi baada ya kupokea fedha zilizotolewa na wizara ya maji kwa ajili ya maboresho hayo.

Akizungumza Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kigoma, Mhe Ahmed Mwilima, ambaye ameiongoza kamati ya siasa ya CCM katika ukaguzi huo, ameeleza kuwa maboresho hayo yanathibitisha thamani ya fedha zilizotumika (value fo maney)na kutoa pongezi kwa uongozi wa KUWASA kwa kusimamia vyema matumizi ya fedha za umma  kwa kulifanya jengo kuwa la kisasa zaidi. 

Amesisitiza kwa kusema maboresho yanalega dhamira ya CCM katika kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kumtua mama ndoo kichwani kwani wananchi watahudumiwa katika  mazingira yaliyoboreshwa.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamezungumzia ubora na umaridadi wa ofisi hizo, na kuuelezea kuwa, kwa sasa utoaji wa huduma ya maji kwa Wananchi wa Kigoma Ujiji umeimarika zaidi. Wameeleza kuwa huduma hiyo imeboreshwa kwa kiasi kikubwa tofauti na hapo awali, hivyo wakazi wa Kigoma Ujiji wanafaidika na utendaji mzuri unaotekeleza ilani ya CCM.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA, Ndugu Poas Kilangi, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, amethibitisha kuwa mpaka sasa, ukarabati umefikia asilimia 98 ya ukarabati huo, na kuongeza kuwa jitihada zaidi zinaendelea kuhakikisha ukarabati huo unakamilika kufikia mwishoni mwa mwezi februari 2024.

Ndugu Kilangi ametoa shukrani kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe Shaban Kilumbe Ng’enda, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za ukarabati ofisi hizo. 

Pia ametoa shukrani za dhati kwa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa jengo la ofisi za KUWASA Kigoma.