Joy FM

Dkt Mpango: Serikali imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji

7 July 2023, 10:32

Makamu wa Rais Dkt. Philipo Mpango akikata utepe wakati akizindua hoteli Bwami Mjini Kasulu, Picha Na Emmanuel Kamangu

Wananchi wazawa wa Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuwekeza katika miradi mbalimbali mkoani humo ili kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Na, Emmanuel Kamangu

Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango amewataka watanzania kutumia fursa ya kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kukuza uchumi wa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

Dk Mpango ameyasema hayo Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati akifungua Hotel ya Bwami Dubai iliyojengwa na mwekezaji mzawa na kusema serikali imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji ikiwa ni sambamba na kuanzisha miradi ambayo wananchi watanufaika nayo.

Makamu wa Rais Dk. Mpango akizindua hoteli ya Bwami Dubai iliyopo Kasaulu Kigoma, Picha na Emmanuel Kamangu

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sitachini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Hassan Suluhu imeondoa tozo na kodi mbalimbali ambazo zilikuwa ni kero kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Sauti ya Makamu wa Rais Dk. Mpango

Naye Mkurugenzi wa hotel ya Bwami Dubai, Evance Chocha ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hali iliyofanya kujenga hotel hiyo ya kisasa katikati ya mji wa Kasulu huku akiomba serikali kutatua cha ngamoto za barabara na umeme ili wawekezaji waweze kushawishika na kuja kuwekeza kigoma.

Sauti ya Mkurugenzi wa Hoteli ya Bwani Dubai