Joy FM

Wanafunzi wafundwa kilimo cha kahawa kibondo

15 April 2024, 12:33

Shamba la Miche ya Kahawa katika kijiji cha Itaba Wilayani Kibondo, Picha na James Jovin

Katika kukabiliana na changamoto za utegemezi kwa wanafunzi baada ya kuhitimu ngazi mbalimbali za elimu nchini kituo kidogo cha utafiti wa kahawa Tanzania TACRI ofisi za kigoma kimeanza kutoa elimu ya kilimo cha kahawa kwa wanafunzi wa sekondari Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.

Na James Jovin

Shule ya Sekondari Itaba iliyoko wilayani Kibondo mkoani Kigoma imefanikiwa kutatua baadhi ya changamoto mbali mbali na kuwafundisha wanafunzi elimu ya kujitegemea kupitia kilimo cha kahawa ili waweze kujitegemea kupitia kilimo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Itaba wameeleza kunufaika na kilimo cha kahawa shuleni hapo na kwamba watahakikisha wanalima zao hilo  hata baada ya kuhitimu masomo yao sambamba na kuisambaza elimu hiyo kwa wananchi wengine

Aidha wanafunzi hao akiwemo Vitus Venance na Yasinta Jeremia wamesema kuwa elimu ya kujitegemea hasa kilimo itasaidia sana wanafunzi wengi wanaomaliza shule na kukaa mitaani bila kujishughulisha na kazi yoyote.

Sauti ya wanafnzi katika shule ya Sekondari Itabata Wilayani Kibondo

Mkuu wa shule ya sekondari Itaba  mwl Magambo Daniel amesema mradi huo wa kilimo cha kahawa  ulianza mwaka 2020 shuleni hapo na kwamba umekuwa na manufaa makubwa ikiwemo kufundisha wanafunzi elimu ya kujitegemea hasa kwa wale wanaohitimu na kushindwa kuendelea na elimu ya juuu.

Meneja wa kituo kidogo cha utafiti wa kahawa Tanzania TACRI ofisi za kigoma  Sophia Malinga ambaye ametembelea shule hiyo na kujionea kazi inayofanywa na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu  amesema Mwikitikio wa wananchi kwa kilimo cha Kahawa ni mkubwa huku Halmashauri ikijipanga kutafuta masoko.