Joy FM
Joy FM
29 June 2026, 13:08

Umoja wa viongozi wa dini ni jambo muhimu sana katika kuleta amani, maadili na maendeleo katika jamii na viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuwaongoza waamini katika njia sahihi zinazompendeza Mungu na pia zinazochangia ustawi wa jamii kwa ujumla
Na Sofia Cosmas
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuacha uadui na badala yake kuungana kwa pamoja katika kuujenga mwili wa Kristo, ili kuwaongoza waamini kuachana na tabia zisizofaa katika jamii na kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Wito huo umetolewa na Mchungaji Jacksoni Maneno wa Kanisa la Christian Labour Church (CLC) wakati wa ibada maalumu ya ufunguzi wa kanisa hilo lililopo mtaa wa Masanga Lubabi, Kata ya Buhanda Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mchungaji Maneno amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa kanisa hilo Kigoma ni kuwavuta watu kumjia Yesu Kristo, kuwaweka huru kutoka katika vifungo mbalimbali na kuwasaidia kumtambua Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
Naye Mkuu wa Chuo cha CLC, Mwl. Milinganyo Nzamu, amesema kumekuwa na msukumo wa kuongeza ujuzi kwa wachungaji, jambo lililowafanya kuanzisha chuo pamoja na kanisa hilo mkoani Kigoma, kwa lengo la kupanua huduma hizo hadi nje ya mipaka.
Baadhi ya waamini waliojiunga na kanisa hilo wanaeleza namna walivyovutiwa na kanisa hilo.
Kanisa la Christian Labour Church limefunguliwa rasmi mkoani Kigoma chini ya Mchungaji Jacksoni Maneno, likianza na washirika 11, wakiwemo watu wazima tisa na watoto watatu.