Joy FM

DC Kibondo ataka wasimamizi wa miradi kuepuka mivutano

7 May 2026, 10:26

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Kanali Aggrey Magwaza, Picha na Mwandishi wetu

Mivutano kati ya wasimamizi wa miradi inaweza kuathiri utekelezaji wa miradi kwa njia nyingi, hasa pale ambapo ushirikiano na mawasiliano yanapokuwa dhaifu

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Kanali Aggrey Magwaza amewataka viongozi na wasimamizi wa miradi wilayani humo kuepuka mivutano ya kisiasa inayoweza kupelekea miradi kutekelezwa kinyume na matarajio

Kanali Magwaza amesema amesema hayo wakati akitoa salamu za serikali kupitia kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa za robo ya tatu ya mwaka 2025/26 ya kuanzia  Januari – Machi 2026

Amesema zipo changamoto ambazo zimeonekana kujitoeza hasa katika miradi ya hisani kutokana na mradi wa barabara ya lami ikiwemo shule ya msingi Busunzu  A ambayo imejengwa mahali ambapo kuna shule nyingine.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Kanali Aggrey Magwaza

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bw. Steven Janks amesema wataendelea kusimamia na kutekeleza maelekezo yote yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi