Joy FM

World vision yakabidhi mradi wa Buhoma kwa serikali Kasulu

31 July 2026, 13:13

Baadhi ya wananchi wakiwa katika hafla ya kukabidhi mradi wa Buhoma, Picha na Mwandishi wetu

Mradi huu umeacha urithi wa miundombinu na huduma muhimu ambazo zikiendelea kusimamiwa vizuri na Serikali pamoja na wananchi, zitaendelea kunufaisha jamii kwa miaka mingi ijayo

Na Mwandishi wetu

Shirika la World vision Tanzania kwa ufadhili wa shirika la World Vision Marekani limekabidhi kwa Serikali mradi wa maendeleo wa  Buhoma ambao umetekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 katika tarafa ya Makere Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Kwa kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu na maji.

Mradi huu wa maendeleo ya wa Buhoma kwa wananchi wa  tarafa ya makere ulianza kutekelezwa na shirika la world vision Tanzania mwaka 2010 ambapo safari yake inahitimishwa rasmi Septemba mwaka huu 2026 ambapo utafikisha miaka 16 huku mwakilishi wa meneja wa Shirika hilo nchini tanzania Steven Nyagonde akisisitiza usimamizi mzuri wa miradi yote iliyotekelezwa katika tarafa hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu, Picha na Mwandishi wetu

Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi simon sirro amesema wataendelea kusimamia miradi yote iliyotekelezwa na shirika hilo kupitia mradi wa Buhoma huku akipongeza mafanikio ya kuongezeka kwa ufaulu katika sekta ya elimu.

Mratibu wa mradi wa maendeleo wa Buhoma kutoka shirika la world vision Tanzania Wilaya ya Kasulu Esther Mushendwa ameeleza baadhi ya miundombinu iliyotekelezwa kwa kipindi cha mradi huo.

Mratibu wa mradi wa maendeleo wa Buhoma kutoka shirika la world vision Tanzania Wilaya ya Kasulu Esther Mushendwa, Picha na Mwandishi wetu

Baadhi ya wananchi kutoka tarafa ya makere wameeleza miongoni mwa manufaa waliyoyapata kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wananchi wakiwa katika hafla ya kukabidhi mradi wa Buhoma, Picha na Mwandishi wetu