Joy FM
Joy FM
30 September 2026, 16:12

Wananchi wa eneo hilo wamewaomba wanajamii wenzao kujenga tabia ya kuwashirikisha watu wao wa karibu yale yanayowasibu kuliko kuchukua hatua za kukatiza uhai wao
Na Emmanuel Kamangu
Mtu mmoja ambaye hajafahamika anayekadiliwa kuwa na umri miaka 40 amekutwa amefariki katika msitu wa asili unaomilikiwa na dini ya Kiislamu BAKWATA uliopo mtaa wa Kisangani kata ya Mwilamvya halmashauri ya mji wa kasulu.
Mtu huyo anayesadikiwa kujinyonga amekutwa akininginia chini ya mti huku kamba aina ya manila ikiwa imeshikilia shingoni hali iliyozua taharuki kwa majirani wa eneo hilo na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa msaada zaidi.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kufika eneo la tukio, Kaimu mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilayani kasulu Nsipector Sipelius Rweyemamu amewaomba wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi huku akiwasihi kuepuka kujichukulia sheria mkononi jambo linalogalimu nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kisangani Bw, Yohana kwegeye akizungumza na wananchi wa mtaa huo ambao wamejitokeza eneo la tukio amewaomba kuendelea kusaidiana kumtambua marehemu huku akiwasihi wamiliki wamaeneo ambayo hayajaendelezwa kuyaendeleza ili kupunguza vichaka vinavyoweza kuhatarisha usalama wa raia.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza eneo la tukio mmoja wao akiwa Bw. Yekonia Kibalumwe wamewaomba wanajamii wenzao kujenga tabia ya kuwashirikisha watu wao wa karibu yale yanayowasibu kuliko kuchukua hatua za kukatiza uhai wao.
Tukio hili limeibua simanzi kwa wananchi wa eneo la serikali ya mtaa wa kisangan kata ya mwilamvya ingawa hatuna budi kukubali kuwa mwezetu ametutoka, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.