Joy FM

Wito wa walimu wenye ulemavu Kasulu kwa serikali

8 October 2026, 10:04

Baadhi ya walimu wenye ulemavu, Picha na Hagai Ruyagila

Walimu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya Kasulu Mkoani wamesema utatuzi wa changamoto zinazowakabili ni sehemu muhumu ya kuweka mazingira rafiki kwao.

Na Hagai Ruyagila

Baadhi ya walimu wenye ulemavu Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za kutatua changamoto zinazowakabili katika mazingira yao ya kazi, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu ya ufundishaji kwa ufanisi zaidi.

Wito huo umetolewa na walimu hao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 5, ambapo kwa mkoa wa Kigoma maadhimisho hayo yamefanyika Oktoba 7, 2026 wilayani Kasulu.

Mwalimu mwenye ulemavu, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya walimu Kasulu

Walimu hao wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohusiana na mazingira ya kazi, jambo ambalo wakati mwingine huathiri utekelezaji wa majukumu yao ya kufundisha na kutoa huduma bora kwa wanafunzi.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kasulu, Mwalimu Elisha Kebelo, amesema chama hicho tayari kimepokea changamoto zinazowakabili walimu wenye ulemavu na kinaendelea kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kasulu, Mwalimu Elisha Kebelo, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kasulu, Mwalimu Elisha Kebelo

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Kigoma, Mwalimu Cresensia Tindwa, amesema chama hicho kitaendelea kushirikiana na Serikali katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo, ili walimu wenye ulemavu waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na bila vikwazo visivyo vya lazima.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Kigoma, Mwalimu Cresensia Tindwa, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Kigoma, Mwalimu Cresensia Tindwa