Joy FM
Joy FM
10 November 2026, 08:32

Wadau wa maendeleo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kujitokeza kuwasaidia vijana kwa kuwawekea mazingira bora na mitaji ili waweze kujikwamua kiuchumi
Na Mwandishi wetu
Wito umetolewa kwa vijana wanaojishughulisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kama maafisa usafirishaji katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kujiepusha na vitendo vibaya ikiwemo wizi baadala yake wawe walinzi katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na mdau wa maendeleo Sonda John mara baada ya kukabidhi jengo kwa vijana wa bodaboda wanafanya kazi katika eneo la Businde mkabara na kiwanda ambapo amesema umoja wao utumike katika kukemea vitendo viovu kwenye jamii.

Aidha amewataka vijana hao kujiepusha na matumizi ya dawa za ku;levya kwani vinasababisha vijana wengi kutofikia ndozo zao.
Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kijiwe cha Sonda John Parking, Khalid Kassim amesema kuwa umoja huo ambao umeanzishwa utasaidia katika kupunguza vitendo viovu iwemo wizi na ukwapuaji wa mali za abiria.
Baadhi ya maafisa usafirishaji wameeleza kumshukuru mdau huo kwa kujitokeza kuwasidia jengo la kufanyia kazi na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia vijana.