Joy FM

Wananchi watakiwa kusafisha na kuzibua mitaro Kigoma

1 October 2026, 14:08

Baadhi ya wananchi na viongozi wakiwa katika zoezi la usafi wa mazingira. Picha na Lucas Hoha

Usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi ya watu, biashara na huduma za jamii ni muhimu katika kuhakikisha mazingira yanakuwa salama.

Na Lucas Hoha

Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma imefanya Usafi wa Mazingira kwa kuzibua mitaro katika Soko la Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji lengo likiwa ni kukabiliana na Mvua za El nino zinazotarajia kuanza kunyesha ili zisilete athari kwenye miundombinu na makazi ya wananchi.

Akizungumza na waandishi wa Habaari Afisa Usafi na Mazingira katika Manispaa hiyo Petronila Gwakila amesema kutokana na tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa wameamua kuzibua mitaro ili Mvua zitakapoanza kunyesha maji yaweze kupita, huku akisisitiza wananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo Jabil Majira amesema mazingira yanapokuwa masafi yanasaidia watu kufanya shughuli za maendeleo, huku akiongeza kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakichafua mazingira bila kuzingatia kuwa inaweka kuleta athari kwao.