Joy FM

DC Kasulu awataka vijana kuwa wazalendo

7 September 2026, 14:04

Washiriki wa kongamano la vijana Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Vijana wametakiwa kufanya kazi kwa bidi na kujishughulisha na kazi zitakazowaingia kipato ili kuepeuka utegemezi

Na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Isaac Mwakisu, amewataka vijana wa Halmashauri ya Mji Kasulu kujiandaa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye kwa kuwa wazalendo, kufanya kazi kwa bidii na kujihusisha na shughuli zenye manufaa kwao na taifa kwa ujumla.

Kanali Mwakisu ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vijana la Halmashauri ya Mji Kasulu, lililofanyika katika Chuo cha Ualimu Kasulu.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa, hivyo wanapaswa kuwa wazalendo na kutumia nguvu, maarifa na fursa walizonazo kujenga maisha yao na kuchangia maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye, amesema kongamano hilo limewapa vijana fursa ya kujadili changamoto zinazowakabili, kubadilishana uzoefu pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto hizo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia Julius Simbeye, Picha na Hagai Ruyagila

Naye Amina Kaniki kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, amewataka vijana kutumia teknolojia na fursa za kidijitali ili kupata taarifa kuhusu fursa zilizopo katika maeneo yao na kuzitumia katika kujiletea maendeleo na kulisaidia taifa kupiga hatua.

Baadhi ya vijana walioshiriki katika kongamano hilo wamesema lwamefahamu fursa zilizopo katika maeneo yao na kupata nafasi ya kubadilishana uzoefu ambao utawasaidia katika kujenga maisha yao.

Washiriki wa kongamano la vijana Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya vijana 1,300 kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Kasulu.