Joy FM

Elimu ndogo ya lishe chanzo cha udumavu kwa watoto

23 May 2024, 09:22

Picha ya wanafunzi wakipewa elimu ya masuala ya lishe kibondo, Picha na James Jovin

Licha ya jitihada mbalimbali za wadau na serikali katika kutoa elimu ya lishe kwa jamii bado tatizo la lishe limekuwa pasua kichwa kwani bado watoto wanasumbuliwa na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa lishe ya kutosha.

Na James Jovin – Kibondo

Idara ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma inaendelea kupambana na maradhi yanayosumbua watoto wenye umri chini ya miaka mitano hasa udumavu, utapiamlo mkali na ukondefu yanayosababishwa kwa kiasi kikubwa na elimu ndogo ya lishe bora katika jamii.

Kaimu afisa lishe wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bi. Juckline Sospeter amebainisha hayo akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe zilizofanyika kuanzia mwezi October mwaka jana mpaka kufikia mwezi march mwaka huu

Aidha amesema kuwa vifo vitokanavyo na maradhi hayo ya utapiamlo mkali, ukondefu na udumavu vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na wazazi kuanza kuelewa umuhimu wa lishe bora licha ya kwamba watoto wenye matatizo hayo bado wapo katika jamii.

Sauti ya afisa lishe wilaya kibondo

Kwa upande wake mganga, Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Dr. Henry Chinyuka amewataka viongozi wa shule za serikali kujifunza namna nzuri ya kuratibu mpango wa chakula shuleni ili kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaoshinda na njaa katika shule hizo.

Sauti ya Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya kibondo

Nae kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Dr. Gabriel Chitupila amesema kuwa swala la baadhi ya watoto kupata chakula shuleni huku watoto wengine wakiwa hawapati chakula sio sawa kwa mstakabali wa elimu na afya kwa ujumla hivyo linapaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa wilaya kibondo