Joy FM

Wezi wa dawa vituo vya afya watinga kwenye baraza a madiwani

9 May 2024, 13:16

Madiwani wilayani kibondo wakiendelea na vikao vya baraza la madiwani, Picha na James Jovin

Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wizi wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya jambo ambalo linakwamisha upatikanaji wa dawa kwa wagonjwa wanapohitaji kutibiwa.

Na James Jovin – Kibondo

Idara ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imetakiwa kushirikisha kamati za afya na kuweka wazi mchakato wa kuhamisha dawa kutoka zahanati moja kwenda zahanati nyingine au kituo cha afya ili kuziba mianya ya wizi wa dawa unaosababisha hasara na changamoto kwa wagonjwa.

Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Kumsenga bwana Ladbrod Lock wakati akichangia hoja katika baraza la madiwani la halimashauri ya wilaya ya Kibondo.

Diwani akiwasilisha ripoti kwenye kikao ca madiwani

Aidha bw. Lock amesema kuwa swala la kuhamisha dawa kutoka zahanati moja kwenda nyingine sio tatizo isipokuwa kamati za afya zinapaswa kushirikishwa ili kuweka wazi mchakato mzima lakini pia kuhakikisha mali ya umma inalindwa.

Sauti ya diwani w kata ya kumsenga

Akijibu hoja hiyo mganga mkuu wa wilaya ya Kibondo Dr. Henry Chinyuka amekili kuwa upo utaratibu wa kuhamisha dawa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine na kwamba atatoa maelekezo kwenye zahanati zote kuhakikisha wanashirikisha kamati za afya katika mchakato huo.

Sauti ya mganga mkuu wa wilaya ya kibondo

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Habili Maseke ameitaka idara ya afya kuhakikisha inarejesha fedha ama dawa zilizohamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine kwa kuwa wananchi wa eneo husika ndio wanapaswa kunufaika na dawa zilizonunuliwa kwa michango yao.

Sauti ya mwenyekiti wa wilaya kibondo mkoani kigoma