Joy FM

Wananchi waipongeza serikali maboresho huduma za afya Kasulu

23 February 2024, 15:37

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa kuongeza idadi ya zahanati, vituo vya Alafya na kuboresha hospital ya wilaya ya Kasulu Mlimani kuhakikisha jamii inapata huduma za afya kwa wakati na kuepuka kutembea umbali mrefu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ambaye ni mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Mh, Prof. Joyce Ndalichako baada ya kutembelea kituo cha afya cha Kiganamo.

Waziri Ndalichako amesema ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ni mpango wa serikali kwa nchi nzima kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya afya ya uhakika.

Prof. Ndalichako

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji Kasulu Dkt. Peter Janga amesema ujenzi wa zahanati na vituo vya afya na uboreshaji wa hospital ya wilaya ya Kasulu imesaidia wananchi kupata huduma za uhakika na kutotegemea hospitali ya wilaya pekee kama ilivyokuwa hapo awali.

Dr Peter Janga

Aidha Dkt. Janga amesema kwa sasa wananchi wa halmashauri ya Mji Kasulu wanapata huduma kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wapo baadhi ya wagonjwa iliwalizimu kusubiri kupata huduma mpaka siku mbili kufuatia changamoto iliyokuwepo mwanzoni.

Dr Peter Janga

Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka halmashauri ya Mji Kasulu wamesema serikali imeendelea kutimiza ahadi yake kwa jamii kupata huduma za afya karibu.