Joy FM

Mafuriko yazihamisha kaya 17 wilayani Kasulu

5 January 2024, 17:38

Takribani Kaya 17 katika mtaa wa Kigungani Kata ya Mwilanvya Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma zimekumbwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hapo jana na kupelekea baadhi ya kaya kuhama.

Moja ya nyumba zilizoathiriwa na mafuriko hayo. Picha na Hagai Ruyagila

Na, Hagai Ruyagila

Mvua hiyo iliyodumu kwa zaidi ya masaa mawili imepelekea baadhi ya nyumba kujaa maji katika mtaa huo huku baadhi ya kaya zikilazimika kuyahama makazi yao.

Wahanga wamafuriko hayo wanaeleza namna walivyokumbana na hali hiyo.

Diwani wa kata ya Mwilanvya Emmanuel Gamuye ameiomba serikali kufanya jitihada za haraka kuzisaidia kaya hizo ambazo zimekubwa na mafuriko.

Naye Mratibu wa maafa kutoka halmashauri ya Mji Kasulu Gregory Shawa amesema uongozi wa halmashauri unafanya jitihada za haraka ili kutatua changamoto hiyo.

Pia Shawa ameiomba jamii inayoishi mabondeni kuhama maeneo hayo ili kukaa katika sehemu salama kuepuka mvua zinazoendelea kunyesha kwani mvua za msimu huu ni nyingi

..