Joy FM

Miundombinu mibovu, uhaba wa vifaa vyaitesa shule ya msingi Rutale

25 October 2023, 13:54

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Rutale wakipokea msaada wa viti kutoka taasisi ya Joy in The Harvest. Picha na Lucas Hoha

Na, Lucas Hoha

Licha ya wadau wa maendeleo na serikali kufanya jitihada za kupunguza uhaba wa miundombinu ya madawati na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Rutale iliyopo kata ya Kipampa manispaa ya Kigoma Ujiji, bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa miundombinu hiyo.

Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Christina Edwin Kasanga mara baada ya shirika la Joy the Harvest kuwasaidia viti 15 vya kukalia na kuomba wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Joy the Harvest na Radio Joy Mwenge Muyombi, amesema wametoa msaada huo baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwasilisha ombi la ukosefu wa viti vya kukalia.

Aidha Muyombi ameongeza kuwa shirika hilo litaendelea kuunga mkono serikali katika kufikisha huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo huduma ya maji safi na salama, kupunguza uhaba wa madawati shuleni na kuwasaidia wanaoishi katika mazingira magumu.