Joy FM

Udamavu kwa watoto kigoma pasua kichwa

22 April 2024, 09:02

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa na wawakilishi wa ubalozi wa marekani wakati wa uzinduzi wa mradi lishe, Picha na Mpiga picha wetu

Viongozi Mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia huduma za afya na lishe kwa usahihi ili kunusuru watoto kuandamwa na tatizo la udumavu licha kuwa ni mkoa unazalisha vyakula vya kutosha

Na Kadislaus Ezekeil – Kigoma

Nchi za Tanzania na Marekani zimezindua mradi wa miaka mitano wa lishe unaolenga kupunguza udumavu kwa watoto waliochini ya miaka mitano, katika mikoa mitano ya Tanzania bara ambayo hali ya udumavu inaonekana kuwa juu na kuathili watoto wengi.

Mradi huo unatekelezwa chini ya shirika la maendeleo la serikali ya marekani USAID na wadau wengine, kwa thamani ya dora za marekani milioni 40, matarajio ikiwa ni kuwa na jamii yenye afya bora.

Sauti ya  Mkuu Wa Mradi Wa Lishe USAID na Mkurugenzi Mtendaji Usaid.

 Viongozi mbalimbali akiwemo katibu tawala mkoa wa Kigoma Hassan Abbas pamoja na mkurugenzi wa mipango na bajeti ofisi ya Waziri mkuu, sera, Bunge na uratibu Eleuter Kihwele, wamesema serikali imekuwa ikipambana kwa ukamilifu Dhidi udumavu, na kwamba mradi huo utachochea mapambano dhidi ya udumavu.

Sauti ya Katibu Tawala Mkoa Wa Kigoma na Mkurugenzi Wa Mipango Na Bajeti Ofsi Ya Waziri Mkuu.