Joy FM
Joy FM
17 June 2026, 21:03

Waamini wa dini ya kikristo na wasio wakristo Mkoani Kigoma wameaswa kuondokana na imani za kishirikina na badala yake kumfanya Mungu kuwa ngome katika maisha yao.
Hayo yamesemwa na Rd Matiasi Kalihadya katika misa takatifu iliyoambatana na ibada ya uzinduzi wa albamu ya “Bwana ni Ngome” ya kwaya ya wito iliyofanyika katika viwanja vya kanisa la mtakatifu Yohane Anglikana Kibwigwa Mkoani Kigoma ambapo amewataka wakristo na wasio wakristo kuacha kuwategemea waganga wa kienyeji kwani mara nyingi huwaacha katika hali ya umaskini.

Aidha amewataka wakristo kuwekeza kwa Mungu kwa kujitoa kwa moyo katika kusaidia kazi ya Mungu kuendelea na kujiwakea akiba katika maisha ya baadae na kuujenga mwili wa kristo
Katika risala kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Katibu wa kwaya Yaledi Isaka, wameeleza kuwa moja ya mafanikio ni pamoja na kuwafanya watu kuja kwa Yesu kama lilivyo agizo la Kristo “enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu”, lakini moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwakwamisha katika kufika maeneo ya mbali na huduma ni ukosefu wa chombo cha usafiri.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Emmanuel Bulaganya amesema kuwa madhehebu ya dini yamekuwa msaada mkubwa katika kukomesha na kuwaelimisha watu wanaoamini iman za kishirikina.
Nao baadhi ya waumin wa Kanisa la Agricani Kibwigwa wamesema maono ya mchungaji ya kumfanya Bwana kuwa ngome yatawafanya kukua na kuondokana na kutegemea waganga
Akihitimisha sherehe hiyo mgeni rasmi Bw Isaak Shinyange ambaye ni mfanyabiashara, ameendesha halambee ya ununuzi wa gari hilo la aina ya kosta na kupata kias cha sh.miloni kumi