Joy FM

Waathirika wa mafuriko wapewa msaada Kigoma

22 April 2026, 16:17

Baadhi ya Msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa kwa wananchi walioathika na mafuriko, Picha na Lucas Hoha

Msaada huu si tu wa kuokoa maisha kwa muda mfupi, bali pia kuwasaidia waathiriwa kujijenga upya na kuwa na uwezo wa kujitegemea tena

Na Mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji waliopoteza makazi yao baada ya kukumbwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa na kusababisha nyumba zao kubomoka.

Pole hizo za Rais Samia zimetolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, wakati wa kugawa misaada ya mahitaji muhimu kwa wananchi waliopatwa na kadhia hiyo kutoka katika kata sita kati ya kata 19 za Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mkuu wa Mkoa Kigoma akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na mnufaika wa msaada huo, Picha na Lucas Hoha

Balozi Sirro amesema ni wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba inazuia hali kama hiyo kuendelea kutokea kwa siku zijazo ikiwemo kuchukua hatua za kuimarisha miundombu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro

Aidha misaada iliyotolewa ni pamoja na unga wa Sembe kilo 1,000, Mchele kilo 1,200, Maharage kilo 800, Sukari kilo 200 Mafuta lita 400 na Sabuni kilo 120, ambapo Balozi Sirro amesema misaada iliyotolewa imewalenga wale waliopata madhara makubwa zaidi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro

Hata hivyo baadhi ya wathirika wa mafuriko hayo wameshukuru kwa msaada huo huku wakiomba serikali kukarabati barabara na maneo yote yalioathirika na mvua hizo.