Joy FM

Kamati yatembelea mradi wa kimkakati Kigoma

15 April 2026, 1:10 pm

Muonekano wa mradi wa ujenzi wa soko la Mwanga ambao umefikia 68% picha na tovuti ya Manispaa ya Kigoma ujiji

Ziara ya Kamati ya Uchumi inaelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha miradi ya kimkakati inaleta matokeo chanya, ikiwemo kuongeza ajira, kukuza uchumi wa ndani, na kuboresha maisha ya wananchi.

Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, elimu na afya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mhe. Gregory Keberezo ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kukagua miradi ya kimkakati inayoendelea kutelelezwa katika Manispaa hiyo.

Wajumbe hao wametembelea na kukagua ujenzi wa soko la Mwanga unaoendelea ukiwa umefikia 68% ya ujenzi, ujenzi wa soko la samaki katika mwalo wa Katonga ukiwa umefikia 39% na ujenzi wa soko la samaki katika Mwalo wa Kibirizi ukiwa hatua ya kujaza kifusi.

Muonekano wa ujenzi wa mradi wa soko katika mwalo wa Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na tovuti ya Manispaa ya Kigoma Ujiji

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Gregory Keberezo amewataka Wataalamu kuendelea kusimamia kikamilifu ujenzi wa miradi hiyo ya uwekezaji na inayoboresha miundombinu na Mazingira rafiki kwa Wafanyabishara na kukuza Mapato ya Halmashauri.

Wajumbe wa Kamati ya uchumi, elimu na afya Manispaa ya Kigoma Ujiji, wakiwa kwenye picha baada ya kutembelea miradi, Picha na Tovuti ya Manispaa ya Kigoma Ujiji