Joy FM
Joy FM
24 July 2026, 09:51

Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii kupitia utoaji wa huduma za afya, elimu, mazingira, kilimo, haki za binadamu na sekta nyingine nyingi hata hivyo, mashirika mengi yamekuwa yakitegemea fedha kutoka kwa wafadhili wa nje, hali ambayo wakati mwingine huathiri utekelezaji wa shughuli zake
Na Hagai Ruyagila
Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Kanali Isaac Mwakisu, ameyataka mashirika yote yasiyo ya kiserikali (NGOs) Wilayani humo kujenga vyanzo mbalimbali vya upatikanaji wa fedha ili kuhakikisha shughuli zao zinaendelea kwa ufanisi hata pale mfadhili mmoja anapositisha au kuondoka katika ufadhili.

Kanali Mwakisu ametoa wito huo wakati akifungua kikao cha robo ya mwaka kuanzia April hadi Juni 2026 cha Jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) wilayani Kasulu
Amesema utegemezi wa mfadhili mmoja unaweza kuhatarisha utekelezaji miradi na utoaji wa huduma kwa wanancha, hivyo ni muhimu kwa mashirika hayo kupanua wigo wa ushirikiano kwa kujenga mitandao na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuimarisha uendelevu wa shughuli na program wanazotekeleza katika jamii.
Kaimu Msajili msaidizi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali halmashauri ya Mji Kasulu Godfrey Jeremiah amesema yapo Mashirika yamekuwa yakishindwa kujiendesha yenyewe kutokana na kutegemea wafadhili ndiyo maana hata mfadhili mwenyewe anapenda kuweka fedha zake sehemu ambayo shirika linaweza kujiendesha lenyewe.

Washirki waliohurulia kikao hicho wameunga mkono hoja ya mkuu wa wilaya ya Kasulu kuhakikisha kila anayeanzisha NGOs anakuwa na uwezo ya kuiendesha kuliko kutegemea zaidi wafadhili jambo ambalo limepelekea baadhi ya NGOs kushindwa kujiendesha zenyewe.