Joy FM
Joy FM
9 September 2026, 11:43

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2026 Wazo Mwang’onda amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya kutolea huduma muhimu kwa wananchi
Na Hagai Ruyagila
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2026 umeanza mbio zake katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ukitokea Wilayani Kibondo ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, barabara na maji inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wilayani Kasulu.


Akisoma risala kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amesema Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani humo utakimbizwa umbali wa kilomita 145.7 na kutembelea jumla ya miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 39.
Kanali Mwakisu amesema katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mwenge wa Uhuru utazindua, kukagua na kutembelea jumla ya miradi 6 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 2 huku miradi 7 katika halmshauri ya Mji Kasulu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 37 ikitarajiwa kutembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi.

Pia amesema watazingatia na kutekeleza maagizo yote yatakayotolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, amesema Mwenge wa uhuru utachochee maendeleo katika wilaya hiyo.
