Joy FM

Wananchi watakiwa kutumia nishati safi kulinda mazingira Kasulu

7 June 2026, 10:15

Katibu tawala Wilaya Kasulu Theresia Mtewele akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira, Picha na Hagai Ruyagila

Wakati leo dunia ikiadhimisha siku ya Mazingira, Wananchi wameaswa kuungana na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo

Na Hagai Ruyagila

Wananchi Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kutunza na kuhifadhi mazingira na kuepukana na changamoto ya ukataji wa miti ambayo inatajwa kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shirika la Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN) Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu, Bi. Theresia Mtewele, amesema ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira nilazima kufanyika mabadiliko na utoaji wa Elimu kwa wananchi.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika hafla ya uzinduzi

Katibu mkuu wa Shirika la Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN), Idrisa Samndeli amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali kuhamasisha wananchi kutumia matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.

Baadhi ya walioshiriki katika uzinduzi huo wamesema elimu waliyoipata itawasaidia kutambua faida za matumizi ya nishati safi ili kulinda mazingira.

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani imebebwa na kaulimbiu isemayo Dira 2050 tuwajibike kukijanisha Tanzania.