Joy FM

Watu 7 hadi 10 hufariki kwa malaria kila mwaka Kasulu

27 April 2026, 14:41

Wananchi na watalamu ngazi yà Halmashauri wakiwa katika zoezi la kusafisha na kufyeka vichaka, Pichaa na Emmanuel Kamangu

Wananchi katika Halmashauriya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti ugonjwa Malaria kwa kuweka salama mazingira na kufukia madibwa katika maeneo yao

Na Emmanuel Kamangu

Imeelezwa watu saba hadi kumi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma hufariki  kila mwaka kutokana na ugongwa wa Malaria.

Amebainisha hayo  mratibu wa kudhibiti ugonjwa malaria katika Halmashauri ya mji wa kasulu Bw. Giribeti  Moshi  katika maadhimisho ya siku ya malaria Dunia maadhimisho ambayo yamefanyika kwa kusafisha maeneo mbali mbali ya mji wa kasulu ikiwemo kufukia madimbwi ambayo ni rafiki na mazalia ya mbu.

Watendaji wa mitaa na kata wakiwa pamoja na Afisa afya mji wa kasulu Bw, Malimi Ntemisemi, Picha na Emmanuel Kamangu

Aidha Bw, Moshi amewasihi sana wanajamii wakiwemo wanafunzi ambao wameshiriki maadhimisho haya kuachana na tabia kutumia dawa pasipo kupima  ikiwemo kuacha tabia ya kutokumaliza dozi wanapobainika kuwa na ugonjwa wa malaria.

Naye afisa afya Halmashauri ya mji wa kasulu Bw, malimi ntemiseni amesema kuna kila sababu ya jamii nzima kwa ujumla kuhakikisha inatambua umhimu wa kusafisha mazingra wanayoishi ili kukabiliana na magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa malaria.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi pamoja na wanachi wakitoa maoni yao baada ya kuhitimisha zoezi la usafi wamesema wanawajibu wa kuendelea kuhakikisha wanafyeka vichaka  na kufukia madimbwi ili kuondokana na ugonjwa hatari wa malaria.

Wanafunzi wa sekondari na wanafunzi wa chuo Cha ualimu kasulu, Picha na Emmanuel Kamangu

Siku ya malaria Duniani huadhimishwa  tarehe 25 April ya kila mwaka  ikiwa ni mkakati wa serikali katika kuendelea kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya njia za kupambana na ugonjwa wa malaria.

Sauti ya Emmanuel Kamangu