Joy FM

Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Uvinza lazinduliwa

22 April 2026, 12:19

Baadhi ya wanawake kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Uvinza wakiwa katika jukwa la wanawake, Picha na Ofisi ya masiliano Uvinza

Wanawake Wilayani uvinza Mkoani Kigoma wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo mikopo ya kuwawezesha kufanya shughali mbalimbali za kiuchumi ili kuwasaidia kuepukana na uchumi tegemezi

Na Mwandishi wetu

Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imezindua rasmi jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika ukumbi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua muhimu ya kukuza maendeleo na ustawi wa wanawake katika jamii.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mh. Dinah Mathamani, amesema jukwaa hilo lina lengo la kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali, kuongeza kipato na kujenga maisha bora kwa familia na jamii kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya Uvinza akizungumza katika mkutano wa jukwa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, Picha na Ofisi ya mawasiliano Uvinza

Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Uvinza, Godfrid Nkuba, amewasihi wanawake waliochaguliwa kutoka kila kata kuhakikisha wanatumia majukwaa hayo kama nyenzo ya kuhamasisha maendeleo, kubadilishana uzoefu, na kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazowanufaisha wanawake wengi zaidi.

Baadhi ya wanawake kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Uvinza wakiwa katika jukwa la wanawake, Picha na Ofisi ya masiliano Uvinza

Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa wanawake wa Wilaya ya Uvinza, kwa kuwapa nafasi ya kujifunza, kushirikiana na kuimarisha uwezo wao wa kiuchumi.