Joy FM
Joy FM
25 June 2026, 11:27

Rushwa ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyoathiri maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla kwa sababu hiyo, juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa zina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha huduma za umma zinatolewa kwa haki na kwa kuzingatia sheria.
Na Sadick Kibwana
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma imepokea na kufanya uchunguzi wa malalamiko 221 ya wananchi katika mwaka wa fedha wa Serikali unaoishia Juni 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kasulu, Elimiliki Kihundrwa, amefafanua kuwa kati ya malalamiko hayo, 12 yamethibitishwa kuwa ni makosa ya rushwa huku malalamiko 7 yakibainika kutohusiana na rushwa.

Aidha, Bw. Kihundrwa amesema baadhi ya tuhuma zinazojitokeza zaidi wilayani humo ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka na ukiukwaji wa taratibu za kiutumishi.INSERT 2 MKUU WA TAKUKURU KSPia Mkuu huyo wa TAKUKURU amebainisha kuwa Sekta ya Ardhi inaongoza kwa malalamiko mengi na changamoto kubwa ni tabia ya baadhi ya wananchi kuridhiana.
Aidha, TAKUKURU Wilaya ya Kasulu imewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu viashiria na vitendo vya rushwa ili kulinda maendeleo ya nchi.