Joy FM

Waziri Aweso akerwa na watumishi wa maji, washidwa kusimamia miradi.

16 July 2023, 14:02

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso katika picha ya ukaguzi wa miradi ya maji Kasulu, picha na Tryphone Odace

Watumishi wa idara za maji Mkoani Kigoma, watakiwa kusimamia miradi kulingana na fedha zinazotolewa na Serikali.

NA, Kadisilaus Ezekiel.

Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso ameagiza kuundwa Tume ya uchunguzi wa miradi ya maji Katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma, kufuatia kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya maji licha ya serikali kutoa fedha za kutekeleza miradi mitatu ya maji.

Mradi wa maji Eneo la Juhudi Halmashauri ya mji Kasulu, Picha na Tryphone Odace

Waziri Aweso amesema hayo katika mkutano wa hadhara mjini kasulu, mara baada ya kukagua miradi ya maji na kuonekana udhaifu mkubwa wa utekelezaji kwa kutumika vifaa visivyo faa katika miradi.

Waziri wa maji akisoma ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maji
Sauti ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amesema Serikali imetoa Bilioni therethini na tano ili kuhakikisha changamoto ya maji inatatuliwa kwa wakazi wa Mji wa Kasulu.

Sauti ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Izack Mwakisu na Mbunge Wa Jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndarichako walilalamikia maji yanayoumika kwa sasa, kwa kuwa na tope na kuhofia usalama wa watumiaji.

Waziri wa maji akiwa na Mbunge wa Kasulu Mjini na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.
Sauti ya mkuu wa wilaya kasulu na mbunge Ndalichako.