Joy FM

Chongolo: CCM itaendelea kuisimamia serikali

27 July 2023, 09:10

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo akizungumza na wananchi Mjni Kigoma, Picha na Tryphone Odace

Chama Cha Mapinduzi kimesema kitaendelea kuhakikisha kinaisimamia serikali katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo ili kufikisha huduma bora kwa wananchi.

Na, Tryphone Odace

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo amesema chama hicho kitaendelea kuisimamia Serikali Kuu katika masuala ya uwekezaji na kupingana na wanaotaka kukwamisha uwekezaji wa bandari kwa kudai ndio chachu ya kuifikisha Tanzania katika uchumi unaolenga kunufaisha watanzania wote.

Katibu Mkuu wa chama hicho Daniel Chongolo amesema hayo katika mkutano wa hadhara mjini Kigoma, uliohusisha viongozi mbalimbali wa serikali na mikoa ya Kigoma na Katavi, mkutano uliolenga kueleza tija ya uwekezaji wa bandari kupitia Serikali ya Tanzania na Falme za kiarabu.

Baadhi wa wananchama wa CCM kutoka Mkoani Katavi wakiwa Mkoani Kigoma katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Picha na Tryphone Odace
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

Kwa upande wao wakuu wa mikoa ya Kigoma na Katavi wamesema uboreshwaji wa Miundombinu ya Bandari ni chachu ya ukuaji wa uchumi kwa mikoa hiyo kupitia nchi jirani.

Sauti ya Wakuu wa mikoa ya Kigoma na Katavi wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

Aidha baadhi ya wananchi wakizungumzia uwekezaji wa Bandari wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu, ili kutoa hofu iliyopo kuwa Bandari zimeuzwa.

Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika Mkutano wa hadhara na katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, Picha na Tryphone Odace
Sauti ya wananchi wakizungumzia uwekaji wa Bandari