Joy FM

Wazazi watakiwa kuwa karibu na watoto, kuwalinda na ukatili

23 October 2023, 12:40

Mji wa Kigoma, Picha na Mtandao

Ili kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaisha kwenye jamii, wazazi na walezi na jamii kwa ujumla wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili kuwakinga na vitendo vya ukatili.

Na Tryphone Odace

Wazazi na walezi manispaa ya Kigoma Ujiji, wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili kutambua mienendo yao ambayo inaweza kusababisha kufanyiwa vitendo vyaĀ ukatili.

Hayo yamebainishwa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi kituo cha Kigoma Mjini Paschal Damas wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Bangwe kwa lengo la kujadili hatua na mikakati ya kukabiliana na vitendo vya ukatlii kwa jamii.

Amesema watashirikiana na serikali ya kata katika kutokomeza ukatili huo dhidi ya watoto na akina mama.

Aidha Diwani wa kata ya Bangwe Saidi Betese amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakihusika na vitendo vya ukatili wa kingono kwa watoto wao lakini taarifa zimekuwa hazitolewi ili wahusika wachukuliwe hatua.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi katika kata hiyo wamekiri vitendo hivyo kufanywa na baadhi ya ndugu wa karibu.

Hayo yanajili wakati zikiwa zimepita siku chache baada ya mtoto mwenye umri wa miaka 6 kusadikika kubakwa na mwanaume wa miaka 45.